Monday, January 3, 2011

JE WAJUA MAJI YA MACHUNGWA,TANGAWIZI NA KITUNGUU SWAUMU VYAWEZA KUTIBU KIKOHOZI

VIFAA:-
Machungwa 3, Tangawizi na Vitunguu Swaumu vikombe 2.

JINSI YA KUTENGENEZA MCHANGANYIKO HUO.
Nawa mikono yako kwa sabuni mara na baada ya matayarisho.

Osha Tangawizi na uhakikishe umetoa tope lote,kisha toa maganda na utwange.

Osha na menya Machungwa ili utomvu wake usiingie kwenye mchanganyiko.Yakate na kamua,maji yake changanya ndani ya tangawizi na vitunguu swaumu ulivyotwanga.

Tikisa mchanganyo huo ndani ya chupa nyingine yenye kizibo,kisha chuja mchanganyiko huo na kichujio cha chai.Unaweza ukaonja na kama ni kali sana unaweza kuweka sukari.

Kunywa mchanganyiko huo bilauri moja asubuhi na jioni,angalia matokeo yake baada ya siku 3


JE WAJUA VITUNGUU MAJI UNAWEZA KUTUMIA KAMA DAWA ?.

Vitunguu maji hutibu magonjwa yafuatayo:-

Uvimbe
Kikohozi
Vidonda vya tumbo
Mifupa
Ngozi
Koo
Figo
Tumbo
Mkojo

MAYARISHO

Menya Vitunguu 3 vikubwa,Visage au vitwange ili upate maji maji yake,kisha changanya kidogo na maji yaliyochemka,Chukua punje 3 za vitunguu swaumu,mwaga maji ya vitunguu maji juu yake.Acha mchanganyiko wake ukae ndani ya bilauri masaa 2,kisha weka asali vijiko 5.
Tumia kunywa mchanganyiko huo,kijiko kimoja kikubwa kutwa mara 3.

UCHUNGUZI WAFANYIKA NA KUENDELEA KUFANYIKA,NA KUDHIHIRIKA KUWA BINADAMU WATAWEZA KUISHI KWENYE SAHARI YA MARS














HII NDIO SAYARI YA MARS


HAPA NI SAYARI YA DUNIA NA MARS.NA HIYO PICHA NYINGINE INAONYESHA JINSI MPANGILIO MZIMA WA SAYARI ULIVYO (ORBIT)
HIKI NDICHO CHOMBO KILICHOTUMWA KWENYE SAYARI YA MARS,KIFAA HIKI KINAITWA NASA PHOENIX LANDER HAPA NDIO KINARUKA. 
HIKI NDIO NASA PHOENIX LANDER,HAPA MIMEJARIBU KUKUONYESHA JINSI
KILIVYOUNDWA NA UFANYAJI WAKE WA KAZI.
HIKI PIA NI BAADHI YA VYOMBO VITUMIKAVYO KUTAFITI
 
UMEMUONA HUYU MSHIKAJI YUPO BUSY ANGANI
Wanasayansi wa kituo cha anga cha nchini Marekani Cha NASA,Mwaka huu kiliamua kupeleka kifaa kilichojulikana kama NASA PHOENIX LANDER kwa nia ya kuchunguza hali ya hewa ya sayari hiyo.
Chombo hicho kilifanikiwa kutua kwenye ardhi ya sayari hiyo na kufanikiwa kurejesha mchanga wa sahari hiyo huku duniani kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Uchunguzi wa wanasayansi hawa una nia ya kulinganisha mazingira ya sayari hiyo kama yanaweza kushabihiana na mazingira ya sayari ya dunia ambako watu wanaweza kuishi.
Uchunguzi huo wa udongo unaotumia vifaa vya kiroboti,umekamilika na sasa wanatarajia kukamilisha uchunguzi wa maji ifikapo septemba.
Tangu taasisi ya NASA kuanza kufanya uchunguzi wake katika sayari ya MARS,hii imekuwa ni mara ya kwanza kuyafikia na kuyaonja maji yaliyomo kwenye sayari hiyo.Huu ulikuwa ni mpango wa kwanza kutangazwa uliokuwa ukiongozwa na Mwanasayansi William Boynton na ulifanikiwa kuchukua mchanga sayarini Mei 25 mwaka huu,ambako alikuwa akitumia kifaa cha PHOENIX LANDER.
Katika uchunguzi huu wa ardhi walifanikiwa kuchunguza na kugundua kwamba ardhi ya huko inaweza kushabihiana na iliyopo duniani kwa baadhi ya sehemu.Uchunguzi huo wa udongo ulifanikiwa vizuri mara baada ya kupelekwa katika maabara ya kikemia,katika tendo lililopewa jina la kifupi la TEGA '' Thermal and Evolved - Gas Analyzer instrument ''.
Wakidhibitisha uchunguzi wao kwenye mkutano kati yao na wanahabari uliofanyika katika chuo kikuu cha Arizona huko Tueson,walidai kwamba wamegundua kuwepo na uwezekano wa kuishi watu katika ardhi ya huko.
'' ... Tumepata ushahidi wa kuwezekana kuishi kwa watu baada ya kupatikana kwa udongo kabla ya kuyaona maji mwezi uliopita na kwamba imekuwa ni mara ya kwanza kwa wanasayansi hao kuyagusa na kujaribu kutumia maji hayo ... ''. Alieleza mmoja wa wanasayansi wa mradi huo Bw William Boynton.
Pia alisema kwamba kifaa chao cha Phoenix Lander kinafanya uchunguzi zaidi katika sayari hiyo ya MARS kikiwa kinaendelea kuchunguza mambo mengine zaidi.
Amedai kwamba pia waliyapata maji mengine yalikuwa katika hali ya barafu ambayo waliyachukua na kuja nayo kwenye maabara na kuyayeyusha,kisha waliyajaribu kwa kunywa.
Pamoja na kwamba katika maeneo mengine wamepata barafu,ila katika maeneo mengine wamepata udongo mkavu,mithili ya ule uliopatwa na ukame.
Ilichukua siku 90 kifaa cha NASA kuchimba na kugundua aina tofauti za maji zilizokuwa chini ya sayari hiyo.Kiongozi mkuu wa mradi huo Peter Smith aliendelea kubainisha kwamba barafu hilo lilipatikana kupitia uchimbaji wa roboti zilizokuwa zikitumia mikono yake
'' ... mara baada ya kuchunguza ndipo tukajua barafu hizo zinaonyesha mwanzo zilikuwa maji na baada ya kukaa muda sana ziliganda na kutengeneza udongo ... '' ,alisema Bw Peter Smith.
NASA pia imetangaza kwamba hivi sasa wapo katika hatua za mwisho za Uchunguzi na wanatarajia ifikapo Septemba mwaka huu watakuwa wamemaliza kuchunguza na kutoa ruhusa ya watu kuishi katika sayari hiyo.