Monday, January 3, 2011

JE WAJUA MAJI YA MACHUNGWA,TANGAWIZI NA KITUNGUU SWAUMU VYAWEZA KUTIBU KIKOHOZI

VIFAA:-
Machungwa 3, Tangawizi na Vitunguu Swaumu vikombe 2.

JINSI YA KUTENGENEZA MCHANGANYIKO HUO.
Nawa mikono yako kwa sabuni mara na baada ya matayarisho.

Osha Tangawizi na uhakikishe umetoa tope lote,kisha toa maganda na utwange.

Osha na menya Machungwa ili utomvu wake usiingie kwenye mchanganyiko.Yakate na kamua,maji yake changanya ndani ya tangawizi na vitunguu swaumu ulivyotwanga.

Tikisa mchanganyo huo ndani ya chupa nyingine yenye kizibo,kisha chuja mchanganyiko huo na kichujio cha chai.Unaweza ukaonja na kama ni kali sana unaweza kuweka sukari.

Kunywa mchanganyiko huo bilauri moja asubuhi na jioni,angalia matokeo yake baada ya siku 3


JE WAJUA VITUNGUU MAJI UNAWEZA KUTUMIA KAMA DAWA ?.

Vitunguu maji hutibu magonjwa yafuatayo:-

Uvimbe
Kikohozi
Vidonda vya tumbo
Mifupa
Ngozi
Koo
Figo
Tumbo
Mkojo

MAYARISHO

Menya Vitunguu 3 vikubwa,Visage au vitwange ili upate maji maji yake,kisha changanya kidogo na maji yaliyochemka,Chukua punje 3 za vitunguu swaumu,mwaga maji ya vitunguu maji juu yake.Acha mchanganyiko wake ukae ndani ya bilauri masaa 2,kisha weka asali vijiko 5.
Tumia kunywa mchanganyiko huo,kijiko kimoja kikubwa kutwa mara 3.

No comments:

Post a Comment